new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya nAnA ya

New Art New Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya Nana Ya-PDF Download

  • Date:20 Dec 2019
  • Views:224
  • Downloads:0
  • Pages:7
  • Size:424.80 KB

Share Pdf : New Art New Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya Nana Ya

Download and Preview : New Art New Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya Nana Ya


Report CopyRight/DMCA Form For : New Art New Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya Nana Ya


Transcription:

new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya nAnA kwa mwaka 2018. new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya nAnA ni mwito unaotolewa kila mwaka kwa. wasanii wenye umri kati ya miaka 18 na 35 mashirika yanayojishughulisha na sanaa na vikundi vya. wasanii kutoka miji ya Wingereza Ethiopia Kenya Ireland ya Kaskazini Rwanda Scotland Sudan ya. Kusini Sudan Tanzania Uganda na Wales nAnA inawapa wasanii fursa kutoka nchi hizi ili waweze. kubuni sanaa mpya kwa kushirikiana kwa pamoja na kufanya maonyesho ya sanaa hizo kwa hadhira. inayotoka katika nchi hizi,Maelezo Muhimu ya nAnA kwa mwaka 2018. 1 nAnA itafadhili miradi mipya 5 kwa mwaka 2018, 2 Kiasi kisichozidi 30 000 kitatengwa kwa ajili ya kila mradi. 3 Wasanii mashirika yanayojishughulisha na sanaa na vikundi vya wasanii kutoka nchi maalum. zilizotajwa hapo juu watatakiwa waungane ili washirikiane kutengeneza kuwezesha au kutayarisha. kwa pamoja sanaa mpya Mifano inayo onyesha namna mbalimbali ya kutafsiri kigezo hiki inapatikana. katika sehemu inayohusu Maswali yanayoulizwa mara kwa mara katika ukurasa wa 4. 4 nAnA ya mwaka 2018 inalenga hasa kusaidia miradi ya wasanii mashirika yanayojishughulisha na sanaa. na vikundi vya wasanii ambavyo tayari vinashirikiana na wenzao wa nchi jirani au vile ambavyo vinataka. kukuza ushirikiano na mahusiano na wasanii wengine Vilevile vikundi vitasaidiwa katika kutafuta. washirika wapya na katika maelezo kuhusu maswali yanayoulizwa mara kwa mara utapata kuona. namna ambavyo British Council inasaidia wasanii kupata washirika kutoka Wingereza na Afrika. 5 Sanaa na mada za aina zote zinakaribishwa,nAnA ya mwaka 2018 Sifa za Mwombaji Waombaji. 1 Maombi yanaweza kutumwa na msanii mmoja au zaidi shirika moja au zaidi linalojishughulisha na. sanaa au kikundi cha sanaa kimoja au zaidi, 2 Kila mradi utatakiwa ujikite zaidi katika utengenezaji wa kipande kipya au kazi mpya ya sanaa. 3 Mradi unaopendekezwa ni lazima uhusishe walau nchi tatu ambazo mbili kati yao ziwe ni za Afrika. Mashariki na ziwe kati ya zile zilizotajwa hapo juu. 4 nAnA imejikita katika kusaidia sekta za sanaa za mijini kutoka nchi zilizotajwa hapo juu wasanii kazi za. sanaa na hadhira wawe na uhusiano na miji, 5 Kila mradi unatakiwa uwe umelenga kuwafikia moja kwa moja watu wenye umri kati ya mika 18 na 35.
na hadhira inayoshiriki kwa njia ya mtandao wa intaneti Dhumuni la nAnA ni kuongeza mwonekano na. ufahamu wa sanaa za leo kutoka Afrika Mashariki na Wingereza Hivyo suala la kuifikia hadhira moja. kwa moja au kwa kupitia mtandao wa intaneti ni muhimu. 6 Wachangiaji wakuu wanaohusika na mradi wanatakiwa wawe na umri kati ya miaka 18 na 35. 7 Miradi hii inaweza kuchangiwa sehemu ya gharama na zaidi ya mfadhili mmoja. 8 Mwombaji anaweza kutuma zaidi ya ombi moja kwenda kwa new Art new Audiences Sanaa Mpya. Hadhira Mpya, 9 Mwombaji aliyepata fedha za nAnA 2016 17 haijalishi kama alishiriki kama mfadhiliwa mkuu au. mdogo anaweza kuomba fedha za nAnA 2018 Hata hivyo mfadhiliwa aliyeshiriki kama mshirika mkuu. wa nAnA 2016 17 hatoweza kufadhiliwa kama mshirika mkuu wa nAnA 2018. 10 Miradi yote itatakiwa itekelezwe na ikamilike ndani ya kipindi cha miezi 12 baada ya kupokea fedha. kutoka British Council, 11 Ili fedha zihidhinishwe ni lazima iandaliwe ripoti ya utekelezaji wa mradi kwa kipindi cha nusu mwaka na. ya mwisho wa utekelezaji Mfumo wa uandishi wa ripoti hizi utawekwa bayana. 12 Mradi utatakiwa usimamiwe na mtu mmoja au shirika moja Lazima wawe na akaunti ya benki na. kitambulisho cha Taifa iliwaweze kupokea fedha Vilevile watakuw na jukumu la kusimamia ripoti ya. mradi ya nusu mwaka na ya mwisho wa mradi pamoja na mawasiliano kwa umma kuhusu mradi. 13 Asilimia 70 ya fedha itatolewa mara baada ya mkataba kutiwa saini na British Council asilimia 30. iliyobaki itatolewa mara baada ya kuwasilisha ripoti ya mradi ya kipindi cha nusu mwaka. Tizama katika kiunganishi hiki iliupate habari juu ya miradi ya nAnA ya mwaka 2016 17. https www britishcouncil org east africa arts projects nana. Vigezo vitakavyozingatiwa kwa waombaji wa nAnA kwa mwaka 2018. Baada ya mchujo wa barua za maombi na uandaaji wa orodha ya watakaofanyiwa usaili jopo la usaili. litakalofuata litauliza maswali 5 ya fuatayo, 1 Je mradi huu unapendekeza utayarishaji wa sanaa mpya ya leo yenye ubunifu. 2 Je sanaa hii mpya iatatengenezwa na maonyesho yake kufanyika kwa kupitia ushirikiano imara kati ya. wasanii mashirika yanayojishughulisha na sanaa na au vikundi vya wasanii katika nchi zilizotajwa. 3 Sanaa hii mpya itaifikiaje hadhira mpya ambayo inashiriki kwa njia ya mtandao wa intaneti na nyingine. inayoshiriki moja kwa moja katika nchi za Wingereza na za Afrika Mashariki Hadhira itakayofikiwa. inaukubwa gani Nini makadirio kwa tarakimu ya idadi ya hadhira inayotegemewa kufikiwa na je. tarakimu hizi ni halisi, 4 Wachangiaji wakuu wasimamizi watayarishaji wasanii waratibu na waombaji katika mradi huu je ni. watu wenye umri kati ya miaka 18 na 35 Na hadhira ya mradi huu je wengi wao ni watu wenye umri. kati ya miaka 18 na 35, 5 Je bajeti ya mradi huu umechanganuliwa na kufanyiwa utafiti wa kutosha na je ni halisia.
Mchakato wa uchaguzi wa nAnA wa mwaka 2018, Iliuweze kutuma ombi lako kwenda kwa new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya utatakiwa. ukamilishe maombi yako kwakupitia fomu ya maombi kwa njia ya mtandao wa intaneti ambayo. inapatikana hapa https www britishcouncil org east africa arts opportunities. Maombi yanayofanywa kwa njia ya mtandao wa intaneti yatahusisha maswali 5 yanayolenga. kuchambua wazo la mradi wako ushirika na ushirikiano na nchi miji iliyotajwa hapo juu pamoja na. washirika wako uliopanga kujenga ufikiaji wa hadhira ratiba na mpango wako wa mawasiliano na. bajeti yako Pia utapata fursa ya kuambatanisha picha au video na nyenzo nyingine ambazo utapenda. Mara baada ya kutuma ombi lako utapata barua pepe ikikufahamisha kuwa ombi lako limepokelewa. Utafahamishwa siku ya Jumatatu 13 August kama mradi wako umepita katika orodha. yawatakaofanyiwa usaili Angalizo hutofahamishwa chochote kama mradi wako haukupita katika. orodha ya watakaofanyiwa usaili Zoezi la usaili litaendeshwa na mameneja wa sanaa wa British. Council katika kila nchi ambako nAnA unatoa ufadhili. Iwapo utakua umefanikiwa kupita katika orodha ya watakaofanyiwa usaili utaitwa katika usaili utakao. fanyika kwa njia ya Skype na zoezi litadumu kwa muda wa dakika 45 hadi saa 1 Utatakiwa uwasilishe. yaliyomo ndani ya barua yako ya maombi kwa kuzingatia maswali 5 yaliyotajwa hapo juu. Waombaji wote waliofanyiwa usaili lakini hawakufanikiwa kupita watapatiwa majibu yao kama. watayaomba, Ratiba ya mchakato wa uchaguzi wa nAnA kwa mwaka 2018. Maombi ya ufadhili yanakaribishwa kuanzia Jumatatu 4 Juni. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumapili 15 Julai saa 6 usiku saa za Wingereza. Mchujo wa kupata orodha ya watakaofanyiwa usaili utafanyika Jumatatu 16 Agosti Jumapili 12. Waombaji waliochaguliwa kufanyiwa usaili watafahamishwa na kuitwa katika usaili Jumatau 13. Usaili kwa njia ya Skype utafanyika kwa wale waombaji waliochaguliwa kufanyiwa usaili Jumatatu 27. Agosti Ijumaa 31 Agosti,Mchujo wa mwisho Ijumaa 14 Septemba. Waombaji wote kufahamishwa matokeo ya usaili Jumatatu 17 Septemba. Malipo kwa miradi Septemba Octoba 2018,Tarehe ya Miradi kuanza 1 Novemba 2018. new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya nAnA Maswali yanayoulizwa. mara kwa mara,Toleo hili limeboreshwa mara ya mwisho 8 Mai 2018.
Je kama sifahamu washirika wangu ni nani katika hatua hii. Kabla ya kutuma pendekezo lako la new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya tunategemea. kuwa waombaji watakuwa wameshafanya uchunguzi na kuchagua washirika watakaofanya nao kazi. katika nchi zilizotajwa Malengo ya Programu ya Sanaa ya British Council katika Afrika Mashariki ni. kujenga uhusiano baina ya wasanii watayarishaji wenye umri kati ya miaka 18 na 35 kutoka Afrika. Mashariki Ilikukusaidia kutafutaj watayarishaji na washirika utakaofanya nao kazi tunapenda kuwapatia. tovuti za British Council zifuatazo ambazo zinaainisha wasanii watayarishaji wanaotekeleza miradi. inayosisimua Afrika Mashariki na Wingereza,Afrika Mashariki na Wingereza. Tovuti ndogo ya Sanaa za Afrika Mashariki www britishcouncil org east africa arts. Sanaa za Afrika Mashariki za ukurasa wa Instagram www instagram com eastafricaarts. Aina za Sanaa za Wingereza, Sanaa za Uoneshi http visualarts britishcouncil org. Usanifu Ubunifu na Mitindo http design britishcouncil org. Fasihi https literature britishcouncil org, Maigizo na Dansi https theatreanddance britishcouncil org. Muziki http music britishcouncil org,Filamu http film britishcouncil org. Aina za Sanaa, Sanaa na Utamaduni wa kidijitali https medium com intersections arts and digital culture in the uk.
Uchumi wa Sanaa http creativeconomy britishcouncil org. Stadi za kitamaduni https www britishcouncil org cultural skills unit. Utamaduni na Maendeleo https www britishcouncil org arts culture development. Kitovu cha ubunifu http creativeconomy britishcouncil org projects hubs. Ukurasa wa Nyumbani wa Sanaa za British Council https www britishcouncil org arts. Angalizo Ilikuhakikisha kuwa waombaji wote wanapatiwa habari sawa British Council haitoweza. kuwaunganisha moja kwa moja waombaji na washirika katika kipindi hiki au kwa ajili ya mwaliko huu. wa new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya, Kwanini ni lazima niwe na umri kati ya miaka 18 na 35. Programu ya Sanaa ya British Council katika Afrika Mashariki inatoa kipaumbele kwa suala la. kuwaunganisha vijana wabunifu kati ya Wingereza na Afrika Mashariki kulingana na mkakati wake katika. ngazi ya kanda http bit ly 2gV6rFz Tunafahamu kuwa mara nyingi hii sio rahisi hivyo tunashauri kuwa. waombaji washiriki na hadhira ya mradi kwa kadri iwezekanavyo wawe wa umri kati ya miaka 18 na 35. Zipo fursa nyingi za kimataifa ndani ya British Council ambazo unaweza kuziomba tizama hapa. https www britishcouncil org arts opportunities, Ni kipi hakifadhiliwa na New Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya. Warsha Mikutano na Kongamano isipokuwa tu pale ambapo kutakuwepo na uhusiano wa moja kwa. moja na uundwaji wa sanaa mpya, Sanaa ambayo tayari ilikwishatengenezwa kabla ya kupata ufadhili wa new Art new Audiences. Miradi ambayo hailengi kufikia hadhira mpya,Nini maana ya Sanaa Mpya. British Council inafanyakazi na aina nane za sanaa Nazo ni Usanifu Mitindo Filamu Dansi na Maigizo. Uchumi wakibunifu Stadi za Kitamaduni Fasihi na Sanaa za Uoneshi. new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya inatafuta miradi itakayotengeneza sanaa mpya kwa. kutumia aina ya sanaa moja wapo au kwakuzingatia zaidi ya aina moja Aidha tanatafuta miradi inayo. hoji aina hizi za sanaa Ambacho hatutaki ni zile kazi za sanaa ambazo tayari zimeshatengenezwa. Ni nchi zipi zinahusika katika mwito huu wa new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya. Katika mwaka 2018 Programu ya Sanaa ya British Council Afrika Mashariki pamoja na mfuko wa new Art. new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya inafanyakazi katika nchi zifuatazo Wingereza Ethiopia. Kenya Ireland ya Kaskazini Rwanda Scotland Sudan ya Kusini Sudan Tanzania Uganda na Wales. Tunafanya kazi katika zile nchi ambako zipo ofisi za British Council pamoja na rasilimali zake. Je mwombaji ni lazima awe raia au mkazi wa nchi zilizotajwa ili aweze kutuma maombi. Waombaji wa mfuko wa new Art new Audiences wanatakiwa wawe raia wa Wingereza Ethiopia Kenya. Ireland ya Kaskazini Rwanda Scotland Sudan ya Kusini Sudan Tanzania Uganda na Wales Waombaji. wanatakiwa wawe na vibali vya kuishi au kufanya kazi katika nchi hizi Washiriki wa mradi wanatakiwa. wawe raia wa nchi hizi Hadhira inayoshiriki katika mradi nao wengi wao wanatakiwa wawe raia wa nchi. hizi lakini wanaweza kutoka nchi nyingine yeyote,Nini Maana ya Hadhira Mpya.
new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya inalenga kuwa chachu kwa hadhira kutoka. Wingereza iliiweze kuona sanaa mpya kutoka kwa wanaAfrika Mashariki na hadhira ya Afrika Mashariki. kuona sanaa mpya kutoka kwa Waingereza new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya inalenga. ile miradi itakayo fanya maonyesho ya sanaa kwa hadhira ambayo wengi wao wana umri wa kati ya. miaka 18 na 35 na ambao hawajawahi kuona sanaa yako Hadhira ambayo ipo siku zote nayo. inakaribishwa lakini pendekezo lako la new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya linatakiwa. lionyeshe namna ambavyo mradi wako utaifikia hadhira mpya kwa ajili ya sanaa yako. Je ninaweza kutuma maombi kama mtu binafsi, Kama unayo akaunti ya benki kitambulisho cha taifa na unaweza kuthibitisha uwezo wako wakusimamia. miradi mikubwa new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya iko tayari kupokea maombi kutoka. kwa watu binafsi Walau nchi tatu zihusike katika mradi na mbili kati yao ziwe nchi za Afrika Mashariki na. hasa zile nchi zilizotajwa katika kitini hiki cha mwombaji. Mradi wangu unatakiwa uanze lini, Miradi yote inayofadhiliwa na new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya inatakiwa ikamilike. ndani ya miezi 12 mara baada ya kupokea fedha, Unamaanisha nini ukisema Wasanii Mashirika yanayojishughulisha na Sanaa na vikundi vya. sanaa ni lazima vishirikiane kutengeneza kuwezesha au kuzalisha kazi mpya ya sanaa. Zipo nyingi ambavyo tunaweza kushirikiana katika utayarishaji wa kazi mpya za sanaa Hapa chini utapata. baadhi ya mifano inayoonyesha namna ambavyo ushirikiano huu unaweza kufanyika. Kikundi cha Sanaa cha Rwanda kitatengeneza kazi mpya ya dansi na wasanii wa sanaa za maonyesho. new Art new Audiences Sanaa Mpya Hadhira Mpya inatafuta miradi itakayotengeneza sanaa mpya kwa kutumia aina ya sanaa moja wapo au kwakuzingatia zaidi ya aina moja Aidha tanatafuta miradi inayo hoji aina hizi za sanaa Ambacho hatutaki ni zile kazi za sanaa ambazo tayari zimeshatengenezwa

Related Books